IQNA

Saudia yaruhusu Ibada ya Umrah baada ya miezi sita

16:56 - October 04, 2020
Habari ID: 3473230
TEHRAN (IQNA) -Kundi la kwanza la Waislamu wanaotekeleza Ibada ya Umrah limeingia leo katika Msikiti Mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah baada ya ibada hiyo kufungwa kwa zaidi ya miezi sita kutokana na janga la corona.

Wizara ya Hija na Umrah Saudia imesema wafanyaziara 6,000 wataruhusiwa kutekeleza Ibada ya Umrah kila siku kwa kufuatilia taratibu maalumu zilizowekwa ili kuzuia kuenea corona. Kwa sasa wanaoruhusiwa kutekeleza ibada ya Umrah ni Waisoamu wanaoishi ndani ya Saudi Arabia.

Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuwa itaanza kupokea wafanyaziara wa kigeni wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ibada ya Umra mwezi mmoja ujao. 

Waziri wa Hija na Umra wa Saudi Arabia, Mohammad Saleh Benten amesema, baada ya miezi 8 ya kusitisha kupokea mahujaji katika miji ya Makka na Madina kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, kuanzia leo Jumapili mahujaji wa ibada ya Umra kutoka ndani ya nchi, na mwezi mmoja baadaye mahujaji kutoka nje ya Saudia wataruhusiwa kufanya Umra lakini kwa kuzingatia masharti. 

3927189

captcha