IQNA

Magaidi 65 wa ISIS wajisalimisha Afghanistan

21:28 - November 01, 2021
Habari ID: 3474500
TEHRAN (IQNA)- Magaidi 65 wa kundi la ISIS au Daesh wamejisalimisha katika mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Pakistan.

Taarifa ya idara ya mkoa wa Nangarhar imesema: “Kupitia upatanishi wa viongozi wa kikabila katika wilaya za Kot na Batkot mkoani Nangarhar, magaidi 65 wa Daesh wamejisalimisha kwa Imarati ya Kiislamu (Taliban) na wamejuta kuhusu vitendo vyao.”

Watu hao sasa wanafuatiliwa kwa karibu na wakikiuka mapatano ya kuwaachilia huru watachukuliw hatua kali, amesema Dkt Bashir, mkuu wa idara ya usalama Nangarhar.

Mkoa huo umekuwa ukishuhudia ongezeko la mashambulizi yanayotekelezwa na magaidi wa ISIS. Mapema mwezi huu serikali ya Taliban ilidai kusambaratisha ngome ya maficho ya magaidi wa ISIS mjini Kabul. Magaidi wa ISIS wamedai kuhusuika na hujuma dhidi ya misikiti ya Mashia wakati wa Sala ya Ijumaa katika miji ya Kandahar na Kunduz ambapo watu zaidi ya 100 wameuawa shahidi.

3476287

captcha