Kwa mujibu wa taarifa msikiti huo wenye ukubwa wa mita mraba 7,000 umejengwa kwa kutegemea misaada ya Waislamu wa zamani.
Sherehe za kufungua msikiti huo zimehudhuriwa na wageni akdhaa rasmi akiwemo mhubiri na msomo wa Kiislamu mwenye asili ya Lebanon ambaye ameishi miaka mingi barania Afrika Sayyid Murtadha Murtadha, Mufti Mkuu wa Zambia Sheikh Asadullah Mwale na Sayyid Muhsin Musavizadeh, mwakilishi wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu nchini Zambia.
Msikiti huo unalenga pia kuwa na kituo cha Kiislamu, ukumbi wa kidini ujulikanao kama Hussainiya na pia kitengo cha elimu.