IQNA

Mchezaji wa Asenali, Thomas Partey, asilimu

16:12 - March 20, 2022
Habari ID: 3475057
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji chipukizi wa timu ya kandanda ya Arsenal ya Uingereza kutoka Ghana, Thomas Partey amesilimu na kuwa Muislamu, kulingana na picha zilizochapishwa na akaunti ya "Muslim Athletes" kwenye mtandao wa Instagram.

Ripoti ya televisheni ya Al jazeera ya Qatar inasema, Partey alionekana kwenye picha akiwa ameshikilia Qur'ani Tukufu na kutabasamu, ingawa yeye mwenyewe hajatoa maoni kuhusu habari hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Wakati huohuo, chanzo cha karibu na kiungo huyo pia kilmethibitisha kwamba nyota huyo wa Arsenal amesilimu na kukubali dini ya Uislamu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Arsenal au The Gunners msimu wa joto wa 2020 kutoka Atletico Madrid kwa muda wa miaka 5, katika mkataba wenye thamani ya euro milioni 50.

Thomas Partey alishiriki na timu ya taifa ya nchi yake, The Black Stars, katika michuano ya hivi karibuni ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ambapo Ghana ilitolewa katika hatua ya makundi.

Partey ni nyota wa pili wa kandanda kusilimu ndani ya wiki chache za karibuni, baada ya nyota wa zamani wa Uholanzi na kocha wa zamani timu ya taifa ya soka ya Cameroon, Clarence Seedorf. 

/3478242

captcha