IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Jisajili ushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Ujerumani

20:30 - October 17, 2022
Habari ID: 3475943
TEHRAN (IQNA) - Wawakilishi kutoka nchi 30 wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Ujerumani mwezi Novemba.

Mashindano hayo yameandaliwa na Shirika la Al-Nour Waqf , yataandaliwa mnamo Novemba 11-13 huko Hamburg.

Danial Abedin, mkuu wa Shirika la Al-Nour Waqf na mkurugenzi wa mashindano, alisema kuwa usajili uko wazi hadi Oktoba 30.

Mashindano hayo yanalenga kuwahimiza Waislamu kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kutekeleza mafundisho yake, alisema.

Kudumisha utambulisho wa kidini, kuimarisha imani ya watu, na kukuza maadili ya Qur'ani miongoni mwa kizazi cha vijana ni malengo mengine ya mashindano hayo, kwa mujibu wa Abedin.

Mashindano hayo yataandaliwa katika kategoria tofauti ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu nzima (kwa walio chini ya miaka 30), kuhifadhi Juzuu 15 (kwa walio chini ya miaka 25), kuhifadhi Juzuu 10 (kwa walio chini ya miaka 18)), na kuhifadhi  Juzuu 5 (kwa walio chini ya miaka 16).

Wale wanaopenda wanaweza kuwasiliana na nambari iliyo hapa chini kupata maelezo zaidi.

International Quran Contest in Germany Set for November

captcha