IQNA

Jinai za Israel

Mpalestina auawa katika shambulio la walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi

23:52 - February 12, 2023
Habari ID: 3476553
TEHRAN (IQNA) – Mwanaume wa Kipalestina ameuawa shahidi na walowezi Wazayuni Waisraeli siku ya Jumamosi katika eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Idadi ya walowezi wa Kizayuni wakiwa wamebeba bastola na mmoja akiwa na bunduki walikaribia kijiji cha Qarawat Bani Hassan ambapo mlowezi mmoja  alifyatua risasi, na kumuua Mpalestina mwenye umri wa miaka 27 aliyetambulika kama Mothqal Rayyan.

Kulingana na waliokuwa katika eneo hilo, wanajeshi wa Israel walifika punde baada ya mauaji hayo kwa lengo la kuwalinda walowezi hao makatili.

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake walitumwa kwenye eneo la tukio baada ya mapigano kuzuka kati ya makumi ya Wapalestina na Waisraeli.

Ukingo wa Magharibi umeshuhudia ongezeko la ghasia tangu Israel ilipozidisha mashambulizi mwaka jana.

Hayo yanaripotiwa wakati ambao, ripoti ya hivi karibuni ilibaini kuwaw wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wamewapiga risasi na kuwaua Wapalestina arobaini na wawili wakiwemo watoto tisa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Wizara ya Afya ya Palestina ilisema katika ripoti yake mpya imesema kwamba idadi ya Wapalestina ambao wameuawa na wanajeshi wa Israel tangu mwanzoni mwa 2023 imeongezeka hadi 42, ikiwa ni pamoja na mwanamke mzee na watoto tisa, wanane kati yao wakati wa Januari pekee.

Ripoti hiyo imesema mwaka huu, utawala wa Israel umefanya jinai nyingi zaidi dhidi ya Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kuliko wakati mwingine wowote katika miaka ya hivi karibuni na kuongeza kuwa, mwaka mpya hadi sasa umekuwa na madhara makubwa kwa watoto Wapalestina.

 

3482445

captcha