IQNA

Jinai za Israel

Wananchi walio wengi Jordan wanapinga uhusiano na utawala haramu Israel

13:48 - February 16, 2023
Habari ID: 3476572
TEHRAN (IQNA) – Idadi kubwa ya watu nchini Jordan wanakataa kutambuliwa kwa utawala wa Israel na uhusiano nao, utafiti mpya unaonyesha.

Katika Kituo cha Kiarabu cha Utafiti na Mafunzo ya Sera chenye makao yake makuu mjini Doha' uchunguzi wa maoni uliopewa anuani ya 'Kielezo cha Maoni ya Kiarabu 2022' mwezi uliopita, ilifichuliwa kuwa asilimia 94 ya wahojiwa wa Jordan walikuwa wanapinga kutambuliwa na uhusiano wowote na utawala haramu wa Israel. Aidha uchunguzi uchunguzi umefanyika katika nchi kadhaa na kubaini kuwa waliowengi katika nchi za Kiarabu wanapinga vikali uhusiano na Israeli ambapo Algeria ni  asilimia 99, Mauritania asilimia 96 nchini Libya asilimia 95, asilimia 92 nchini  Iraq na asilimia 90 nchini Tunisia.

Katika semina katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati cha Chuo Kikuu cha Jordan mnamo Jumatatu, matokeo ya utafiti yalibainishwa zaidi na naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Kiarabu cha Utafiti na Mafunzo ya Sera, Mohammad Al Masri.

Kukataa kwa umma wa Jordan kuitambua Israel, alisema, kunatokana na ukweli kwamba Israel inachukuliwa kuwa ni "mkoloni" na pia ni utawala "ubaguzi wa rangi" ambao una malengo ya kujitanua na kuteka ardhi zaidi za Waarabu na hivyo wananchi wa Jordan wanauona utawala kuwa tishio kubwa la usalama kwa eneo hilo.

Masri pia iliangazia ukweli kwamba baada ya Israel, asilimia 87 ya raia wa Jordan wanaichukulia Marekani kuwa tishio kubwa zaidi kwa eneo la Asia Magharibi.

3482500

captcha