IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ujumbe wa Taifa siku ya Bahman 22 ulikuwa ni istikama na kuunga mkono Mapinduzi kikamilifu

17:49 - February 15, 2023
Habari ID: 3476567
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutana na maelefu ya watu kutoka mji wa Tabriz na kusisitiza kuwa: "Ujumbe wa taifa katika matembezi ya Bahman 22 (11 Februari) ulikuwa ni istikama na kuunga mkono Mapinduzi kikamilifu"

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo Jumatano amekutana na maelfu ya wananchi wa Tabriz na kusema,  watu wa eneo la Azerbaijan ni wabeba bendera ya umoja na uhuru wa Iran.  Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa: "Hamasa hii ya kweli, yenye shauku na iliyojaa maana ni matokeo ya kutopotoshwa  taifa na pia ni ishara ya istikama ya taifa katika mkondo wa Mapinduzi."

Amesema njia hii  ya ustawi na nguvu itaendelea kwa umoja wa kitaifa. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Taifa, bila ya kuhisi uchovu na kukosa matumaini na bila ya kuogopa mapigo, vitisho na mashambulizi ya adui, liliendelea na njia iliyonyooka kwa kuhifadhi utambulisho wake, shakhsia na adhama yake, na katika njia hii, tarehe Bahman 22  mwaka huu, lilifika mitaa ya nchi nzima na kwa motisha mbalimbali lilionyesha uvumilivu wa maana na ukaidi kwa adui."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Vyombo vikubwa vya habari vya Marekani na Kizayuni vinajaribu kuzuia sauti hii kubwa isifikie masikio ya mataifa mengine, lakini wale wanaopaswa kuisikia yaani vyombo vya kutunga sera za Marekani na Uingereza na katika mataifa mengine, mashirika ya kijasusi ya adui, bila shaka walisikia sauti hii. 

Ayatullah Khamenei akiashiria mashambulizi na tuhuma za mara kwa mara za adui kuhusu ulazima wa Iran kutokuwa na nguvu za kijeshi amesema: "Nchi inapiga hatua za ustawi  katika nyanja nyinginezo zikiwemo za viwanda, masuala ya miundombinu kama vile ujenzi wa barabara na ujenzi wa mabwawa na katika nyanja nyinginezo mara nyingi inawekeza zaidi kuliko masuala ya ulinzi, lakini adui, ambaye katika propaganda zake kuhusu ndege zisizo na rubani za Iran ameonyesha hofu yake, anakanusha matukio mengine ya ustawi anangazia tu masuala ya ulinzi."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia kuwepo udhaifu mkubwa katika nchi kubwa na zilizoendelea zikiwemo Marekani, Uingereza na Ufaransa na kusema nchi hizo zimeonyesha udhaifu katika katika masuala kama vile umasikini, maradhi, ubaguzi na ukosefu wa uadilifu wa kijamii.

Katika mkutano huu, Ayatullah Khamenei vile vile ametukuza imani, bidii na utakasifu wa watu wa Tabriz na Azerbaijan na akasema mwamko wa Bahman 29 mjini Tabrizi ulijiri "wakati wenye kuainisha hatuam na siku hiyo ilikuwa siku ya mabadiliko katika historia ya Iran".

4122268

captcha