IQNA

Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani, fursa kwa nchi za Kiislamu Kukutana Pamoja'

17:21 - April 04, 2023
Habari ID: 3476809
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran ameyataja Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kama fursa kwa nchi za Kiislamu kukusanyika pamoja na kunufaika na mafundisho ya Kiislamu na Qur'ani.

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili aliyasema hayo katika hafla ya kuzindua sehemu ya kimataifa ya toleo la 30 la maonyesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa kadhaa kutoka nchi za Kiislamu, akiwemo Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Elimu Asilia wa Mauritania Dah Ould Sidi Ould Amar Taleb na Mohammed Hamid, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Sanaa wa Niger.

Esmaeili amebainisha kuwa wanaharakati wa Qur'ani na wasanii kutoka nchi 21 wanashiriki katika toleo la 30 la maonyesho hayo.

Ameashiria kustawi kwa shughuli za Qur'ani nchini Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 na kusema kuwa, leo hii kuna mamia ya maelfu ya wahifadhi wa Qur'ani na watu wengine wengi zaidi wanaoshiriki katika nyuga tofauti za Qur'ani hapa nchini.

Waziri wa Utamaduni na Miongozi ya KiislamuIran aidha ameashiria hatua dhidi ya Qur'ani Tukufu na matukufu mengine ya Kiislamu katika miaka ya hivi karibuni na akasema hatua zitachukuliwa katika maonyesho hayo kwa lengo la kukabiliana na hatua hizo sambamba na kuendeleza utamaduni wa Qur'ani Tukufu.

Int’l Quran Exhibition An Opportunity for Muslim Countries to Come Together: Iran Culture Minister  

Waziri wa Utamaduni, Utalii na Ufundi wa Niger katika hotuba yake amewashukuru maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kumualika kwenye maonyesho hayo ili kuimarisha umoja kati ya nchi hizo mbili.

"Tuko hapa kukuza utamaduni wa Qur'ani, Uislamu na kuwa Waislamu," alisema, akibainisha kuwa Niger ni nchi ya Afrika Magharibi yenye idadi kubwa ya Waislamu.

Niger inajivunia Uislamu na ina chuo kikuu kikubwa zaidi cha Kiislamu barani Afrika, Mohammed Hamid alisema, akibainisha kuwa hatua kubwa zimepigwa katika nchi yake kuendeleza utamaduni wa Kiislamu na kueneza umaanawi.

Int’l Quran Exhibition An Opportunity for Muslim Countries to Come Together: Iran Culture Minister  

Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Elimu Asilia wa Mauritania pia amehutubia katika hafla ya uzinduzi huo na kuwashukuru viongozi wa Iran kwa kuandaa maonyesho hayo katika mwezi wa Qur'ani Tukufu, yaani Ramadhani, kwa ajili ya kutangaza Kitabu Kitukufu na mafundisho yake.

Pia alisema kuialika Mauritania kushiriki katika maonyesho hayo kunaashiria uhusiano mzuri na wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili za Kiislamu.

Wasanii na wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 21 zikiwemo Pakistan, Iraq, India, Russia, Tunisia, Algeria, Indonesia, Sri Lanka, Oman, Lebanon, Afghanistan, Malaysia, Kenya na Russia wanashiriki katika sehemu ya kimataifa ya maonyesho hayo.

Int’l Quran Exhibition An Opportunity for Muslim Countries to Come Together: Iran Culture Minister  

Tafsiri ya Qur'ani Tukufu, mashairi na fasihi, msikiti wa kutengeneza ustaarabu, maisha ya familia na Qur'ani, watoto, mashauriano ya msingi wa Qur'ani, taasisi za Qur'ani za msingi, elimu ya Qur'ani n.k.

Hafla hiyo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa lengo la kuendeleza fikra za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na pia katika uga wa kimataifa.

Inaonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini humo na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

4131220

captcha