IQNA

Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran

Rais wa Iran ahudhuria sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya 30 ya Qur'ani ya Tehran

14:59 - April 02, 2023
Habari ID: 3476799
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yamefunguliwa rasmi Jumamosi na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi.

Maonyesho hayo yameanza katika siku ya 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kauli mbiu ya maonyesho hayo ambayo yataendelea  hadi tarehe 26 ya Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani ni “Ninakusoma” kwa lengo la kuhimiza  umuhimu wa kuendelea kusoma Qur’ani Tukufu.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa lengo la kukuza utamaduni wa Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini na katika uga wa kimataifa.

Maonyesho hayo huwa na mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani Tukufu nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali huonyeshwa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Sehemu ya watoto na "bustani ya aya" ni miongoni mwa sehemu kuu za maonyesho ya mwaka huu na zimepanuliwa mara tatu ikilinganishwa na maonyesho yaliyotangulia. Aidha vipindi mbalimbali pia vimepangwa kwa ajili ya sehemu ya wanawake na wasichana.

Nchi 22 zinatazamiwa kushiriki katika sehemu ya kimataifa. Zaidi ya hayo, mawaziri wa utamaduni na wakfu kutoka nchi saba wanatazamiwa kutembelea hafla hiyo.

Kulingana na makadirio, hadi vifurushi 5,000 vya futari vitasambazwa miongoni mwa wageni ambao watakuwa aktika ukumbi wa maonyesho wakati wa futari. Idadi hiyo inatarajiwa kufikia 15,000 usiku wa Qadr.

Akizungumza kuhusu kuenziwa watumishi wa Qur’ani Tukufu katika maonyesho hayo, Rais Ebrahim Raisi alisema: Leo ni siku yenye baraka kwani tumejumuika pamoja na watumishi wa Qur'ani Tukufu, wafasiri, watarijumani na wale ambao wamejitolea kwa ajili ya Qur’ani Tukufu maishani. Baraka ziwe juu yao na wale walioifanya Qur’ani kuwa sehemu ya maisha yao, wakahifadhi na kusoma Qur’ani na wakazifahamu aya zake na wakawa ni wenye kutekeleza mafundisho yake.”

Rais wa Iran ameashiria aya za Mwanza za Sura ar-Rahman, zisemazo “Arrah'man, Mwingi wa Rehema, Amefundisha Qur'ani, Amemuumba mwanaadamu,” amesema kuwa Qur’ani Tukufu ni dhihirisho la rehema za Mwenyezi Mungu.

4130873

 

captcha