IQNA

Hujjatul Islam Hamid Shahriari

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yanaweza kukabiliana na propaganda dhidi ya Ushia

16:58 - April 12, 2023
Habari ID: 3476855
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema Maonyesho ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ni mwitikio mzuri kwa chuki dhidi ya Iran (Iranophobia) na chuki dhidi ya madhehebu ya Shia Shiaphobia).

Hujjatul Islam Hamid Shahriari ametoa maoni hayo katika mahojiano na IQNA wakati wa ziara yake katika Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran.

"Kwa kuzingatia kwamba Qur'ani Tukufu ndio msingi mkuu wa madhehebu ya Kiislamu, maonyesho ya Qur'ani yanaweza kuwa chombo chenye ushawishi katika kufikia ukuruba wa madhehebu na kutambua umoja tunaotaka kuupata katika ulimwengu wa Kiislamu," alisema.

Msomi huyo alisema kuwa madole ya kibeberu yanatumia mbinu mbalimbali zikiwemo za chuki dhidi ya Ushia ili kuzusha mifarakano miongoni mwa Waislamu.

"Suluhisho la kukabiliana na njama hizi ni kuwa na shughuli za Qur'ani kwa njia ya maonyesho na matukio mengine yanayofanana na hayo," alisema.

Kwa mujibu wa Shahriari, ushiriki wa wasanii na wanazuoni mashuhuri kutoka mataifa mengine ya Kiislamu unaweza kuandaa mazingira ya kuongezeka maingiliano kati ya nchi za Kiislamu.

Aidha alibainisha kwamba “kwa bahati mbaya, kuna propaganda nyingi dhidi ya madhehebu ya Shia kama baadhi ya watu wanavyodai kimakosa kwamba Mashia  hata wana nakala maalum la Qur'ani.”

Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA) Musalla tarehe 1 Aprili na sehemu yake ya kimataifa ilizinduliwa siku mbili baadaye.

Sehemu ya kimataifa itaendelea kwa siku kumi.

Wasanii na wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi 21, zikiwemo Pakistan, Iraq, India, Russia, Tunisia, Algeria, Indonesia, Sri Lanka, Oman, Lebanon, Afghanistan, Malaysia, Kenya na Russia wanashiriki katika maonyesho hayo.

4133262

captcha