IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Gereza la Algeria lawaenzi wafungwa 150 waliohifadhi Quran

11:05 - April 24, 2023
Habari ID: 3476907
TEHRAN (IQNA) – Gereza moja katika mji mkuu wa Algeria, Algiers limewaenzi wafungwa 150 ambao waliweza kuhifadhi Quran Tukufu kikamilifu.

Wafungwa hao wameenziwa ikiwa ni  sehemu ya toleo la 13 la mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kwa wafungwa yaliyofanyika katika mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Zaidi ya wafungwa 10,000 walikuwa wameshiriki katika shindano hilo ambalo lilifanyika katika makundi matatu, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi na usomaji wa tarteel.

Wakati huo huo, mamlaka za mahakama zitasamehe au kubadilisha hukumu za baadhi ya wafungwa walioshika nafasi za juu katika shindano hilo.

4136060

captcha