IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Washindi wa mashindano ya Qur'ani India waenziwa

15:17 - May 01, 2023
Habari ID: 3476944
TEHRAN (IQNA) - Katika hafla iliyofanyika Lucknow, mji mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh nchini India, washindi wa mashindano ya usomaji wa Qur'ani na Adhan wameenziwa.

Wavulana na wasichana wapatao 120 kutoka sehemu mbalimbali za jiji walikuwa wameshiriki katika mashindano hayo ambayo yaliandaliwa kwa ajili ya watoto na vijana na Taasisi ya Utamaduni ya Muammil ya Lucknow.

Washindani wakuu walipokea medali, vyeti vya heshima na zawadi zingine kwenye hafla hiyo.

Mashindano hayo yalijumuisha usomaji wa aya kutoka kwa Qur'ani Tukufu na Hujjatul Islam Manzar Abbas Shafiei na usomaji wa shairi la kusifu Kitabu Kitukufu la mshairi Saber Ali Omrani.

Watoa mada katika hafla hiyo, Hujjatul-Islam Musa Riza Yusufi na Hujjatul-Islam Saeed al-Hassan Naqavi walisisitiza umuhimu wa kujifunza Qur'ani na kuwapongeza wazazi wa waliofanikiwa katika mashindano hayo ya Qur'ani.

4137565

captcha