IQNA

Jamii

Waislamu wameelekea eneo ambalo si kibla kwa miaka 40 katika msikiti mmoja Uturuki

18:11 - August 10, 2023
Habari ID: 3477411
TEHRAN (IQNA) - Mwaka mmoja uliopita, ilifichuliwa kwamba qibla cha msikiti wenye umri wa miaka 40 katika Wilaya ya Gurcamlar ya Milas, Mugla, nchini Uturuki kilikuwa na makosa. Mwaka mmoja uliopita, ilifichuliwa kwamba qibla cha Msikiti wa Gurcamlar Mahallesi, uliojengwa katika miaka ya 1980, kilikuwa kimeelekea eneo ambalo si Makka.

Ombi lilitumwa kwa Mufti wa Wilaya ya Milas baada ya kubainika kosa ambalo waumuni katika msikiti waligundua kupitia chombo cha satelaiti mwaka mmoja uliopita. Waumini wanaosali hapo walipogundua kuwa kibla cha msikiti huo kilikuwa na makosa mwaka mmoja uliopita kupitia satelaiti, alitoa taarifa kwa Mufti wa Wilaya ya Milas.

Mufti wa Wilaya ya Milas alifanya uchunguzi unaohitajika juu ya malalamiko hayo na kubaini kuwa qibla cha msikiti uliojengwa miaka 40 iliyopita kilikuwa na makosa.

Kwa kuwa kazi ya ubomoaji ilifikiriwa kuwa nzito, upande wa qibla uliainishwa katika mazulia na jamii ya msikiti imekuwa ikisali katika mwelekeo mpya wa qibla kwa mwaka mmoja sasa.

Kati ya masharti muhimu ya Sala katuka Uislamu ni Muislamu kuelekea Qibla, katika mji mtakatifu wa Makka.

4161195

Kishikizo: qibla msikiti
captcha