IQNA

Pepo Katika Qur'ani/2

Kudiriki baraka za Peponi ni zaidi ya uwezo wa ufahamu wa mwanadamu

18:22 - January 29, 2024
Habari ID: 3478274
IQNA – Baraka ambazo waumini watazipata peponi hatuwezi kuzifahamu na kuzidiriki kikamilifu kwani akhera ni dunia iliyo bora zaidi, kubwa na ya juu kuliko dunia hii.

Ndiyo maana tunaweza tu kuwa na wazo au dhana kuhusu  baraka hizo kwa kulinganisha na baraka na raha za ulimwengu huu.

Kwetu sisi, watu tulio katika ulimwengu huu mdogo, kuelewa vipimo vya baraka peponi au Jannatul Firdaus  ni vigumu sana, hata haiwezekani. Tofauti kati ya dunia hii na peponi mbili ni kama tofauti kati ya tone la maji na mto.

Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 35 ya Surah Qaaf: “Humo (peponi) watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada."

Pepo ya milele iliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wa imani na Taqwa (kumcha Mungu) ni habari njema kuhusu Ghayb (yasiyoonekana  na mwanadamu) na kamwe mtu hawezi kufahamu thamani na dhati yake katika dunia hii. Haiwezekani kutambua kiwango cha furaha na saada ambayo mtu atapata kutokana na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu.

Ndiyo maana watu wanaambiwa tu kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu juu ya kutoa thawabu hizo ni ya hakika:

"Isipo kuwa walio tubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote. Bustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wake katika siri. Hakika ahadi yake hapana shaka itafika." (Aya za 60-61 ya Surat Maryam)

Pepo hiyo inaitwa mabustani (katika hali ya wingi) katika aya hii inaonyesha kuwa ina bustani zisizohesabika zilizojaa baraka kwa waumini wachamungu. Ni bustani za kudumu na zenye baraka na wala si kama bustani  za dunia hii ambazo huisha siku moja.

Mojawapo ya wasiwasi mkubwa juu ya baraka za ulimwengu huu ni ukweli kwamba hatimaye zitaisha, lakini hakuna wasiwasi kama huo juu ya baraka za milele peponi.

Neno ‘waja’ katika aya hii linawahusu wale tu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na neno 'katika siri' au ghaibu linahusu ukweli kwamba wanaamini katika kile wasichoweza kukiona. Nukta nyingine hapa ni kwamba baraka za pepo ni kwamba hakuna macho yameziona na masikio hazijasikia kuhusu wao ni nini hasa. Hivyo pepo ni zaidi ya mawazo yetu na ufahamu wetu.

3486994

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu qiyama
captcha