IQNA

Kadhia ya Palestina

Sheikh al-Qaradaghi ahimiza nchi za Kiislamu kuunga mkono Kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel ICJ

15:45 - March 13, 2024
Habari ID: 3478502
IQNA - Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kuunga mkono kikamilifu Afrika Kusini katika kesi yake ya kisheria dhidi ya utawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)

Akizungumza na Shirika la Anadolu, Sheikh Ali Mohiuddin al-Qaradaghi alisema hatua ya nchi za Magharibi kuunga mkono wa mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza ni dalili tosha kuwa nchi za Magharibi kati hazizingatii kanuni za maadili ya kibinadamu.

Akibainisha kuwa utawala haramu wa Israel umefanya jinai kubwa dhidi ya Wapalestina, ikiwemo mauaji ya wanawake na watoto, uharibifu wa hospitali na misikiti, na kuzuia kupelekwa kwa misaada katika Ukanda wa Gaza, amesema historia haijawahi kushuhudia maafa ambayo ulimwengu unashuhudia huko Gaza leo.

Alitoa wito kwa mataifa ya Kiislamu na nchi nyingine na mashirika ya kibinadamu kuunga mkono Afrika Kusini katika kesi dhidi ya Israel.

Mwishoni mwa 2023, Afrika Kusini iliwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu vita vya mauaji ya kimbari ya utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Katika uamuzi wake wa muda wa Januari 26, mahakama ya Umoja wa Mataifa iliamua kwamba hoja za Afrika Kusini zina ukweli. ICJ iliamuru kuchukuliwa hatua za muda, ikisema kuwa utawala wa Israel lazima utekeleze hatua za kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Aidha Sheikh Al-Qaradaghi ametoa wito kwa Waislamu kufanya wawezalo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwahurumia na kuwasaidia watu wa Gaza wanaoteseka kwa njaa, kiu na maradhi.

Alisema anayetaka kufanya Umrah, ambayo ni Mustahab (kitendo kinachopendekezwa lakini si cha lazima), badala yake atoe fedha hizo kuwasaidia watu wa Gaza.

Mkuu huyo wa Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS)  pia alitoa wito wa kuwepo kwa Waislamu kwa wingi katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem).

Israel ilianzisha vita vyake vya mauaji ya kimbari Gaza mnamo Oktoba 7, 2023. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, wapalestina wasiopungua 31,045 wameuawa na 72,654 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel. Takriban asilimia 72 ya waathiriwa ni watoto na wanawake.

Zaidi ya miezi mitano ya mashambulizi ya kikatili ya Israel pia yamesababisha njaa kali miongoni mwa Wagaza.

Takriban watu 25, wengi wao wakiwa watoto, wamekufa kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini katika ardhi ya Palestina katika siku za hivi karibuni.

Utawala katili wa Israel umezuia kuingia kwa chakula na vifaa vya msaada Gaza na kudhoofisha huduma zake za afya.

3487541

Habari zinazohusiana
captcha