iqna

IQNA

lebanon
Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misaada yake na kwamba, haikusita hata kidogo kuisaidia Lebanon.
Habari ID: 3475296    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/26

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu kwa munasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi Sayyid Mustafa Badruddin na kusema kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikuwa ni pigo kwa nchi za Kiarabu na mataifa yote ya eneo.
Habari ID: 3475271    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amewashukuru na kuwapongeza watu wote walioshiriki katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni na akasema ushiriki mkubwa wa Wa lebanon katika uchaguzi huo na matokeo yake yamefikisha ujumbe wa uungaji mkono kwa Hizbullah au Muqawama na silaha zake.
Habari ID: 3475268    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah ameashiria uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni na kusema tatizo la waliowengi nchini Lebanon si silaha za Hizbullah au Muqawama bali ni hali ya maisha.
Habari ID: 3475230    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/10

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa wito kwa Umma mzima wa Kiislamu kuanzisha harakati kubwa zaidi dhidi ya kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Sweden.
Habari ID: 3475143    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/19

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema hali ya ndani ya utawala ghasibu wa Israel u na matukio ya kimataifa yote kwa pamoja yanaashiria kuangamia utawala huo katili.
Habari ID: 3474968    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/24

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah imetangaza kuwa ndege yake moja isiyo na rubani au drone aina ya "Hassan" imeingia hadi ndani ya anga ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina la Israel na kutekeleza oparesheni ya kukusanya taarifa za siri.
Habari ID: 3474945    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/19

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Hizbuallah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amezilaani nchi za Waislamu ambazo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kuutaja utawala huo kuwa ni ‘utawala wa muda’ ambao unaelekea kusambaratika.
Habari ID: 3474934    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/16

TEHRAN (IQNA)- Ikiwa imesalia siku chache kabla ya kumbukumbu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Solemani, mchoro mkubwa wa kamanda huyo na wanajihadi wenzake waliouawa shahidi umepandisha katika barabara kuu inayolekea uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon.
Habari ID: 3474725    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/26

TEHRAN (IQNA)-Klipu ya qarii maarufu wa Lebanon Ustadh Hamza Mon’em akisema baadhi ya aya za Sura Aal Imran katika Qur'ani Tukufu imesambaa katika mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3474653    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/08

TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Habari wa Lebanon George Kordahi amejiuzulu ili kupunguza mgogoro wa nchi yake na Saudi Arabia baada ya kauli yake ya kukosoa vita vya Saudia dhidi ya Yemen.
Habari ID: 3474634    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/03

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuliweka jina la Hizbullah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi hakutaathiri hata chembe azma na irada ya muqawama au mapambano.
Habari ID: 3474609    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/27

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, mazoezi kijeshi yanayofanywa mara kwa mara ya na utawala haramu wa Israel ni kielelezo cha wasiwasi na woga wa utawala huo mkabala wa Lebanon
Habari ID: 3474544    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/12

TEHRAN (IQNA)- Katika kulalamikia matamshi yaliyotolewa siku ya Ijumaa na George Kurdahi , Waziri wa Habari wa Lebanon aliyekosoa uvamizi wa Saudi Arabia na Imarati huko Yemen na kuutaja kuwa usio na maana, Saudia imemwita nyumbani balozi wake mjini Beirut na kumtaka balozi wa Lebanon pia aondoke nchini humo mara moja.
Habari ID: 3474498    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/01

TEHRAN (IQNA)-Saudi Arabia imemwita nyumbani balozi wake wa Lebanon na kumtaka balozi wa nchi hiyo pia aondoke mjini Riyadh, likiwa ni jibu kwa matamshi ya ukosoaji aliyotoa waziri wa habari wa Lebanon kuhusiana na uchokozi na uvamizi wa kijeshi uliofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen.
Habari ID: 3474493    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/30

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema chama cha Al-Quwwatul-Lubnaniyyah (Lebanese Forces) kinalenga kuibua vita vya ndani nchini humo.
Habari ID: 3474442    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/19

TEHRAN (IQNA)- Siku tatu za maombolezo zimetangaza nchini Lebanon baada ya watu saba kuuawa na wanamgambo wakati wa maandamano ya jana katika mji mkuu Beirut.
Habari ID: 3474425    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/15

TEHRAN (IQNA)- Duru za habari nchini Lebanon zimeripoti kuwa mapigano makali yanendelea baina ya askari usalama na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut ambapo idadi ya waliouawa sasa ni sita na waliojeruhiwa ni zaidi.
Habari ID: 3474422    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/14

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amelitaka Baraza la Mawaziri la nchi hiyo ya Kiarabu liombe kufutiwa vikwazo vya kuagiza mafuta kutoka Iran ili yawasaidia wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3474413    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/12

TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kuhusu matukio ya karibuni kabisa ya kisiasa ya nchi hiyo na eneo.
Habari ID: 3474395    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/08