iqna

IQNA

daesh
Wanajeshi Wairaqi wamekuwa na kikao maalumu cha kusoma Qur’ani katika huko Saad al A’adhim katika mkoa wa Diyala, eneo ambalo wamelikomboa hivi karibuni kutoka kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3470483    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/29

Waandamanaji Berlin
Maandamano yamefanyika nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Berlin, Ujerumani ambapo washiriki wameilaani Saudia kwa kuendelea kutoa misaada kwa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.
Habari ID: 3470314    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/15

Mfalme Abdullah II wa Jordan ameituhumi Uturuki kuwa inahimiza misimamo mikali eneo la Mashariki ya Kati sambamba na kueneza magaidi bara Ulaya.
Habari ID: 3470219    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/28

Donald Trump, mwanasiasa wa chama cha Republicans amesema baadhi ya waitifaki wa Marekani, ikiwemo Israel, wanaliunga mkono na kulipa misaada kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3463979    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/16

Idadi ya raia wa kigeni waliojiunga na makundi ya magaidi wakufurishaji nchini Syria wameongezeka maradufu, amesema mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Uingereza.
Habari ID: 3461648    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/09

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia ametangaza hali ya hatari ya siku 30 kufuatia shambulizi dhidi ya basi lililokuwa limewabeba maafisa usalama wa nchi hiyo hapo .jana
Habari ID: 3457119    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/25

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, jinai za kuogofya za makundi ya magaidi kama vile kukata vichwa na kuwachoma moto watu ni dalili ya kuwa mbali kabisa na Uislamu magaidi hao.
Habari ID: 3455805    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/22

Ayatullah Ahmad Khatami
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa wiki mjini Tehran amesema kundi la kigaidi la Daesh au ISIS matakfiri kwa ujumla ni mamluki wa Wazayuni ambao wametumwa kwa lengo la kuwagombanisha Waislamu.
Habari ID: 3454898    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/21

Watu wasiopungua 160 wameuawa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris Ijumaa usiku katika mashambulizi yanayosadikiwa kuwa makubwa zaidi nchini humo tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Habari ID: 3448027    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/14

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la ugaidi lililofanywa na kundi la kitakfiri la ISIS au Daesh nchini Lebanon siku ya Alhamisi ambapo watu 43 waliuawa na wengine zaidi ya 240 wamejeruhiwa.
Habari ID: 3447662    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/13

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limelaani vikali hujuma ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3388672    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/18

Mufti Mkuu wa Tunisia amesema kuwa mirengo yenye kufurutu ada na makundi ya kitakfiri kama ISIS au Daesh ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3386403    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/17

Rais wa Iran na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu wametoa ujumbe tofauti kufuatia kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Hussein Hamedani katika vita dhidi ya magaidi na kutoa mkono wa pole kwa wananchi wa Iran.
Habari ID: 3383361    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/09

Magaidi wa kundi la ISIS au Daesh wameshambulia kwa bomu Masjid Nur jana Jumanne katika mtaa wal al-Nahda katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a ambapo watu saba wamepoteza maisha.
Habari ID: 3382986    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/07

Sayyid Hassan Nasrallah
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa upuuzaji na uzembe wa utawala wa Aal Saud ndio chanzo kikuu cha kujiri maafa ya Mina na kupoteza maisha maelfu ya mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3382979    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/07

Waislamu 25 wa madhehebu ya Shia wameuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a baada ya bomu kulipuka ndani ya msikiti wakati wa Swala ya Idul-Adh’ha mapema leo asubuhi.
Habari ID: 3367085    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/24

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Nickolay Mladenov Mashariki ya Kati amesema kunahitajika muungano wa kimatiafa wa kijeshi ili kuangamiza kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3363344    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/16

Maulamaa Waislamu zaidi ya 1,000 nchini India wametoa Fatwa ya pamoja kulaani na kupinga kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na kusema harakati za kundi hilo ni dhidi ya mafundisho ya Kiislamu.
Habari ID: 3361079    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/10

Maulamaa Waislamu Ghana
Maulamaa wa Kiislamu nchini Ghana wametangaza msimamo wa kupinga vikali kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kutoa wito kwa vijana nchini humo kuisoma na kufahamu ipasavyo tafsiri ya Qur'ani kwa njia sahihi ili wasitumbukie katika mtego muovu wa ISIS.
Habari ID: 3360612    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/08

Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limetekeleza miripuko ya mabomu kwenye msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kupelekea waumini wasiopungua 32 kupoteza maisha.
Habari ID: 3357626    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/03