IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Mauritius

11:10 - May 07, 2016
Habari ID: 3470298
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yamefanyika hivi karibuni nchini Mauritius.

Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya Hassan ibn Thabit nchini Mauritius kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya hqmi.org imeripoti kuwa mashindano hayo yalikuwa na washiriki 29 waliohifadhi Qur'ani katika vitengo vya wanawake na wanaume.

Halikadalika kulikuwa na kategoria tatu za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 15, Juzuu 3 na Juzuu 1.

Sherehe za kuwatunuku zawadhi waliofuzuz zilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Mauritius pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani na wasomi kadhaa wa Qur'ani Tukufu.

Waliozungumza katika hafla hiyo walisisitiza umuhimu wa Qur'ani na umoja wa Waislamu sambamba na kujifunza na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani.

Jamhuri ya Mauritius ni kisiwa kilicho katika Bahari ya Hindi yapata kilomita 2,000 kusini mashariki mwa pwani ya Afrika.

Waislamu ni asilimia 20 ya watu wote wa Malayasia. Waislamu wa Mauritisu ni wenye asili ya India lakini kuna idadi kubwa waliosilimu kutoka kaumu ya Creole.

Kishikizo: mauritius
captcha