IQNA

Kufuatia janga la corona

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yataka mateka Wapalestina waachiliwe huru

15:47 - April 17, 2020
Habari ID: 3472675
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa taasisi za za kisheria Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kuchukua hatua za dharura za kuwaokoa mateka Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa, jumuiya hiyo pia imetaka jamii ya kimataifa isaidia katika kuwatumia dawa na vifaa vya kitiba Wapalestina hao wanaoshikiliwa mateka katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel ili waweze kukabiliana na ugonjwa wa corona.

Katika taarifa iliyotolewa kwa mnasawa wa Siku ya Wafungwa Wapalestina, Jumuiya ya nchi za Kiarabu imeutataka  utawala wa Israel uwaachilie huru Wapalestina wafungwa wazee, wagonjwa na wengine wote walio katika hatari ya kuambukizwa corona.

Tarehe 17 Aprili katika kalenda ya Palestina ni 'Siku ya Mateka wa Kipalestina'. Kwa mujibu Abdul Nasser Farawneh, mkuu wa Idara ya Utafiti katika Kamati ya Masuala ya Mateka na Wafungwa wa Zamani Wapalestina, hivi sasa kuna Wapalestina 5,800 wanaoshikiliwa katika jela za  utawala wa Kizayuni wa Israel na miongoni mwao kuna wanawake 62 na watoto 200.Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yataka mateka Wapalestina waachiliwe huru

Mateka hao Wapalestina wanakabiliwa na mateso na mashinikizo makali kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Moja ya tafauti kubwa za jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mateka Wapalestina na Wapalestina wengine ni kuwa mateka hao huwa katika eneo la kijiografia linalodhibitiwa kikamilifu na utawala wa Kizayuni. Kwa msingi huo, utawala wa Kizayuni huwatesa wafungwa hao kimwili na kisaikolojia. Kwa mfano, utawala wa Kizayuni wa Israel umewahukumu mateka 540 wa Kipalestina vifungo vya maisha mara moja au mara kadhaa.

Hivi sasa kufuatia kuenea ugonjwa hatari wa corona katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu yaani Israel, kadhia ya kufariki mateka Wapalestina inajadiliwa kwa kina na wanamapambano wa kupigania ukombozi wa Palestina.

Hadi sasa mateka wanne Wapalestina wanaoshikiliwa katika gereza za Israel wameambukizwa corona. Imedokezwa kuwa moja ya sababu kuu ya kuenea ugonjwa wa corona miongoni mwa wafungwa Wapalestina ni ukosefu wa matibabu, kutumwa  kwa makusudi madaktari Wazayuni wenye corona katika gereza hizo na pia kuwepo askari gereza walioambukizwa corona ambao nao pia wameachwa kwa makusudi waendelee kufanya kazi.

Mahmoud Abbas, Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametaka jamii ya kimataifa na taasisi za kibinaadamu ziushinikize utawala wa Kizayuni kuhusu hali ya mateka wa Kipalestina.

3892162

captcha