IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /66

Toba ya Dhati; Njia Bora ya Kurejea Kwa Mwenyezi Mungu

16:12 - March 11, 2023
Habari ID: 3476689
TEHRAN (IQNA)- Mwanadamu amezungukwa na dhambi nyingi zinazomweka mbali na Mwenyezi Mungu na zinazomzuia kuwa na hali ya kiroho. Hilo hupelekea mwanadamu kuchanganyikiwa na kupoteza kusudi la kweli la maisha. Njia pekee ya kutoka katika hali hii na kufikia wokovu ni kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Surah At-Tahrim ya Qur'ani Tukufu, njia bora ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu ni toba ya kweli.

At-Tahrim ni Sura ya 66 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 12 na iko katika Juzuu ya 28. Ni Madani na ni sura ya 108 ya Qur'ani  iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad  (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Tahrim (kukataza, kupiga marufuku) lililotajwa katika Aya ya kwanza. Inahusu nadhiri ya Mtume (SAW) ya kujiharamishia kitu ambacho ni Halali, kwa kutaka radhi za wake zake.

Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura ya 1)

Kisha Mwenyezi Mungu anawaita waumini wajilinde nafsi zao na familia zao kutokana na moto wa jahanamu na wakumbuke kwamba watalipwa kwa matendo mema wanayoyafanya hapa duniani.

Sura pia inawahimiza wakosefu watubu na kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Katika sura hii, taubat an-nasuh- (toba ya kweli) imetajwa kuwa ni toba iliyo bora zaidi. Ni toba kamili isiyo na kurudi katika dhambi. Maneno ya toba ya Nasuh, yaliyotajwa tu katika Sura hii, ni neno ambalo lina nafasi maalum katika utamaduni wa Kiislamu.

Taubat an-nasuh-inamaanisha kujaribu kutafuta njia bora ambayo itatumikia masilahi ya mtu. Inatokana na Ikhlas (usafi wa nia). Ni toba itakayomtakasa mtu na kumzuia asirudi katika dhambi.

Katika aya za Sura At-Tahrim, wake wa Nuhu (AS) na Lut (AS) wametajwa kuwa ni makafiri wawili na mke wa Firauni anatajwa kuwa ni mfano wa Muumini mwema na mchamungu ambaye ni mke wa asiyeamini. Pia inamtaja mwanamke aliyeamini ambaye hana mume (Mariamu (SA)).

Inaonekana kwamba mifano hii imetajwa ili waumini wasishangazwe na matendo yasiyofaa ambayo wake za manabii wanaweza kufanya.

Inaweza pia kudhaniwa kuwa uhusiano wa kifamilia hauwezi kuhakikisha wokovu wa mtu kama vile kuwa mke wa Nuhu (AS) na Lutu (AS) hakujawaokoa wanawake hao. Kwa upande mwingine, mke wa Firauni, kwa sababu ya tabia na mwenendo wake safi, alifikia wokovu na Mariamu (SA), ambaye hana mume, alifikia hadhi ya juu na akawa mfano wa kuigwa kwa waumini kutokana na imani na usafi wake.

captcha