IQNA

Idul Fitr

Watoto Kiislamu nchini Kanada wajumuika katika siku ya Idul Fitr

21:46 - April 23, 2023
Habari ID: 3476904
TEHRAN (IQNA) - Kwa watoto katika jamii ya Waislamu wa eneo la St. John nchini Kanada, Jumamosi ilikuwa siku ambayo walijumuika pamoja baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakati maelfu ya waumini wa jumuiya za Waislamu wa Newfoundland na Labrador walikusanyika kwa Sala ya Idi na maadhimisho katika Techniplex huko St John mnamo Ijumaa, Jumamosi ilikuwa siku kwa watoto wa Waislamu kuwa na furaha ya katika eneo hilo.

Watoto mia kadhaa, wakifuatana na wazazi wao, walihudhuria hafla hiyo, na majumba ya tafrija na michezo mbali mbali.

"Hawawezi kusubiri kwenda kwenye ukumbi wa micheo, kuruka, na kupata nishati hiyo huko, kwa furaha," Ayse Akinturk, ambaye alisaidia kupanga shughuli hizo alisema.

"Idul Fitr ni muhimu sana kwa Waislamu kote ulimwenguni na haswa kwa Waislamu wanaoishi katika sehemu hii ya ulimwengu yaani na Newfoundland na Labrador," alisema Akinturk.

Akinturk alisema matukio kama haya ni mazuri kwani yanaonyesha idadi Waislamu wa eneo hilo ambao ni kutoka kaumu na rangi mbalimbali.

"Watu ambao asili yake ni kutoka sehemu tofauti za ulimwengu, lakini ni Waislamu wa Canada wameusanyika kwa furaha."

3483314/

captcha