IQNA

Waislamu Kanada

'Waache Watoto Wetu': Waislamu wamlaani Waziri Mkuu wa Kanada kwa matamshi yanayoibua mgawanyinyiko

21:43 - September 26, 2023
Habari ID: 3477655
OTTAWA (IQNA) – Shirika moja la Kiislamu nchini Kanada (Canada) limelaani matamshi ya "uchochezi" na "mgawanyiko" yaliyotolewa na wanasiasa wa Kanada, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Justin Trudeau, dhidi ya matakwa ya haki ya watu wanaopinga mtaala wa itikadi ya kijinsia shuleni ambao lengo lake na kupotosha watoto kimaadili na kifamilia.

Katika taarifa ya Jumatatu, Jumuiya ya Waislamu wa Kanada (MAC) ilishutumu vikali matamshi dhidi ya maandamano ya;oyotolewa hivi majuzi  na baadhi ya wanasiasa, akiwemo Waziri Mkuu.

"Kwa kutaja maandamano ya amani ya maelfu ya wazazi wanaohusika kuwa eti ni ya kueneza chuki, viongozi wa Kanada na bodi za shule wanaweka mfano hatari wa kutumia nafasi yao ya ushawishi kuharibu familia bila haki, na kuwatenga wanafunzi wengi," ilisema.

Kauli hiyo inakuja huku maelfu ya wananchi wa Kanada wakiwemo Waislamu wakiandamana Septemba 20 kupinga itikadi ya jinsia inayofundishwa madarasani. Maandamano ya Watu  Milioni 1 Kwa Ajili ya Watoto yalifanyika katika miji na miji 102 kote Kanada.

Waandamanaji walionyesha upinzani wao kwa mipango ya mafunzo ya shule kuhusu elimu ya ngono ambayo ni pamoja na itikadi ya kijinsia, na vyoo mchanganyiko shuleni. Waandamanaji hao pia walisema kwamba vijana hawapaswi kuhamasishwa kukumbatia taratibu za matibabu zinazobadili jinsia ambazo zingewatia makovu maishani.

Maandamano hayo ya amani yalitia ndani ishara nyingi, kuanzia "Waache Watoto Wetu Pekee Yao" na "Elimu sio Zoezi la Ulazimishaji Itikadi" na "Demokrasia sio udikteta" na "Wacha wavulana wawe wavulana na wasichana wawe wasichana."

Trudeau aliingia kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani wa Twitter) siku ya Jumatano, akishutumu maandamano hayo kama kitendo cha "chuki".

MAC ilibainisha kuwa "maelfu ya Waislamu, wakijumuika na vikundi vingine vya kidini, waliandamana ili kuelezea wasiwasi wao, wakitaka haki zao kama wazazi kuhusiana na elimu ya watoto wao."

Habari zinazohusiana
captcha