IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /83

Sura ya Qur'ani inayowaonya walaghai

21:08 - June 10, 2023
Habari ID: 3477127
Katika sheria za Kiislamu na katika jamii za Kiislamu kuna kanuni maalum za shughuli za kiuchumi na adhabu kali hutolewa kwa wale wanaofanya makosa ya kiuchumi kama vile ulaghai.

Adhabu za makosa hayo si kwa wale walio katika dunia hii pekee, kwani Mwenyezi Mungu, katika Sura Al-Mutaffifin, anawaonya walaghai kwamba wao pia wataadhibiwa Siku ya Kiyama au Siku ya Hukumu.

Al-Mutaffifin ni jina la sura ya 83 ya Qur'ani Tukufu, ambayo ina aya 36 na iko katika Juzuu ya 30. Ni Sura ya 86 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Ilikuwa ni Sura ya mwisho iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) huko Makka kabla ya Hijra (kuhama) kwake Madina.

Mwenyenzi Mungu anawaonya Al-Mutaffifin- wale wanaofanya udanganyifu- katika aya ya kwanza, na hivyo jina la sura linatokana na watu hao. Surah hii inawaonya wasivuruge mfumo wa uchumi wa jamii kwa ulaghai wao kwa sababu vinginevyo wataadhibiwa Siku ya Kiyama kwa kitendo hicho.

Aya ya 1 hadi 3 inahusu wenye kufanya ulaghai au wapunjao na kukanyaga haki za watu katika kufanya biashara, ikisisitiza kwamba vitendo hivyo ni Haramu (vimekatazwa kidini) na miongoni mwa madhambi makubwa.

" Ole wao hao wapunjao!  Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.  Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza." Alu Mutaffifin (1-3).

Kisha Sura inaelezea Siku ya Kiyama na sifa zake, ikimaanisha makundi mawili ya watu, yaani wale wanaofanya wema na walio karibu na Mwenyezi Mungu na wafanyao maovu. Inasema kuwa katika dunia hii makafiri waliwacheka Waumini lakini Siku ya Kiyama Waumini watawacheka makafiri.

Katika Aya ya 7 hadi 21, makundi matatu ya watu yametajwa: Fujjar (watenda maovu) wanaoikadhibisha Siku ya Kiyama; Abrar (wafanyao wema) walio karibu na Mwenyezi Mungu na wanapata baraka peponi; Na Muqarrabin (walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu) ambao nafasi yao ni ya juu kabisa, na kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, hao ni watu wa Yaqin (yakini).

Katika dunia hii makafiri wasioamini Siku ya Kiyama na Akhera wanawafanyia maskhara Waumini. Kwa mujibu wa Surah hii, “Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. (Aya ya 12) Allamah Tabatabai ameandika katika Tafsiri ya Al-Mizan ya Qur'ani Tukufu kwamba Aya hii inaonyesha jambo pekee linalomzuia mwanadamu kufanya madhambi ni kuamini Siku ya Kiyama na kwamba mwenye kutumbukizwa katika madhambi hufika mahali akakanusha Siku ya Kiyama.

 

Habari zinazohusiana
captcha