IQNA

Mjue Imam Hussein -Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake- (AS)

Sababu za Mwamko wa Ashura kwa kuzingatia marejeo ya Qur'ani ya Imam Hussein (AS)

22:42 - July 22, 2023
Habari ID: 3477323
TEHRAN (IQNA) – Tangu mwanzo wa safari yake ya kwenda Makka na kisha Karbala, Imam Hussein (AS) alisoma aya za Qur’ani Tukufu katika nyakati tofauti.

Kuzingatia maudhui ya aya alizosoma wakati wa safari kunatusaidia kupata taswira bora zaidi ya malengo ya Imam Hussein (AS) katika mwamko  wa Ashura, mwanazuoni wa kidini Najaf Lakzaei.  Hii ni sehemu ya hotuba yake kwenye kongamano la ‘Uchambuzi wa Mtazamo wa a Qur’ani Tukufu wa Imam Hussein (AS) Katika  Mwamko Wake’.

Kuna vipengele vya kisiasa katika aya za Qur’anI Tukufu  ambazo Imam (AS) alizisoma. Kuna idadi kubwa ya aya alizosoma na haba tutaangazia baadhi tu ya aya hizo.

1- Alipomkabili Marwan: Wakati mtawala wa Madina, kwa amri ya Yazid, alipomtaka Imam Hussein (AS) akule kiapo cha utii kwa Yazid, Imam (AS) alisoma Aya ya 156 ya Surah Al-Baqarah: “…Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” Kisha Imam Hussein(AS) akasema kwamba kama utawala wa serikali hii utaendelea, Uislamu utaangamizwa. Kisha akasoma Aya ya 33 ya Surah Al-Ahzab: “…Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara.” Kisha kaongeza kwamba,  “Sisi ni familia iliyotakasika na hatuwezi kuweka kiapo cha utii kwa mtu kama Yazid.”

2- Wakati wa kuingia Makka: Imam Hussein (AS) alipofika Makka, alisoma Aya ya 22 ya Sura Al-Qasas: “Alipoanza (Musa) safari ya upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu Mlezi akaniongoa njia iliyo sawa."

3- Alipotoka Makka: Imamu Husein (AS) alisoma Aya ya 21 ya Sura Al-Qasas: “Basi (Musa) akatoka, naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Akasema: Mola wangu Mlezi! Niokoe na watu madhaalimu.” Hapa Imam (AS) kwa kusoma Aya hii analinganisha hali aliyonayo na hali ya Musa (AS).

4- Aliposikia khabari ya kuuawa shahidi Muslim bin Aqil: Imam (AS) alisoma Aya ya 23 ya Sura Al-Ahzab: “ Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” Kwa mujibu wa aya hii, baadhi ya waumini walikufa kishahidi na kundi la pili wanangojea kuuawa kishahidi.

5- Aliposikia msaada wa Ubaidullah ibn Hurr Jaafi: Ubaidullah ibn Hurr Jaafi hakukubali mwaliko wa Imam (AS), akisema hatafuatana na Imam (AS) lakini atakuwa tayari kusaidia. Imam Husein (AS) akasoma aya hii: “Sikuwalingania (madhalimu) kushuhudia kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.” (Aya ya 51 ya Surah Al-Kahf)

6- Wakati wa kukabiliana na Ibn Abbas: Mmoja wa wale waliojaribu kumzuia Imam (AS) asianzishe mwamko alikuwa Ibn Abbas. Kulikuwa na mazungumzo baina yake na Imam Hussein (AS) kuhusu Bani Ummayah ambapo Imam (AS) alisoma Aya ya 54 ya Sura At-Tawbah: “ Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila nao wamechukia.” Aya hii inawaelezea wanafiki.

7- Wakati Hurr alipoanza kuziba vyanzo vyote vya maji ili maji yasimfikia Imam Hussein (AS) na masahaba zake, Imam (AS) alisoma Aya ya 41 ya Sura Al-Qasas: “Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa.”

Hurr na jeshi lake walipaswa kutambua kwamba kwa kusoma aya hii, Imam Hussein (AS) anawaelezea Yazid, Ibn Ziyad na wengineo mbele yao kuwa ni wale wanaowalingania watu motoni huku Imam (AS) akiwalingania watu kwenye nuru.

3484435

captcha