IQNA

Arbaeen 1445

Waandishi wa habari 600 wa kigeni kufika Iraq kuakisi matembezi ya Arbaeen

14:58 - August 24, 2023
Habari ID: 3477484
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya waandishi wa habari 600 kutoka nchi mbalimbali wataangazia matukio yanayohusiana na matembezi ya kila mwaka ya Arbaeen nchini Iraq.

Tawfiq al-Habali, mkurugenzi wa idara ya vyombo vya habari na mawasiliano ya Gavana wa Karbala, alisema waandishi wa habari, wapiga picha watakuja Iraq kwa ajili ya tukio hilo kubwa la kidini kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu, Kiislamu na zisizo za Kiislamu.

Alisema kituo cha vyombo vya habari chenye mtandao wa kasi sana kimeanzishwa katika mji mtakatifu wa Karbala ili kuwakaribisha wanahabari kutoka Iraq na nchi nyinginezo wakati wa msimu wa Arbaeen.

Al-Habali alibainisha kuwa kituo hicho kina vyumba mbalimbali vya habari kwa ajili ya vyombo vya habari.

Mpango wa kina wa vyombo vya habari umebuniwa kwa ajili ya kuangazia ibada ya Ziara ya Arbaeen inayotarajiwa kufikisha ujumbe wa Arbaeen na mwamko wa Imam Hussein (AS) kwa walimwengu, aliendelea kusema.

Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo maana yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu.

Baada ya kufa shahidi Imam Hussein (AS) mikononi mwa katili Yazid bin Muawiya, watu ambao walishangazwa na ukatili wa ukoo wa Ummaya walianza kuzuru kaburi lake kutoa heshima zao na tokea wakati huo hadi leo vizazi katika umma wa Kiislamu vimeendeleza utaratibu huo. Kila mwaka idadi ya wafanyaziara katika Siku ya Arabeen inaongezeka ambapo mwaka uliopita idadi hiyo ilivunja rekodi na kufika milioni 21.

 

Habari zinazohusiana
captcha