IQNA

Wanigeria wahuisha Arubaini ya Imam Hussein AS

12:58 - December 14, 2014
Habari ID: 2618158
Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria jana waliungana na Waislamu wengine duniani na kushiriki kwa wingi katika maombelezo ya Arubaini ya Imam Hussein (A.S) kwa kukusanyika katika mji wa Zaria.

Sheikh Ibarahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria aliwaambia waandishi habari katika hafla hizo kwamba, mahudhurio yalikuwa makubwa mno na kwamba Imam Hussein alitaka kuleta mabadiliko katika Umma wa Kiislamu wakati huo ambapo Usilamu ulipaswa kutakaswa.  Maombelezo ya Arbaini ya Imam Hussein (A.S) mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW yalifanyika pia katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan na India.

Nchini Iraq mamilioni ya wafanya ziara kutoka ndani na nje ya Iraq walikusanyika katika mji mtukufu wa Karbala na kushiriki katika mambolezo hayo muhimu.../mh

2618063

captcha