IQNA

Arabeen 1445

Vyombo vya habari kimataifa vinapuuza tukio la Arbaeen

15:57 - August 20, 2023
Habari ID: 3477468
TEHRAN (IQNA) – Mamilioni ya watu kutoka duniani kote wanaelekea katika tukio la kila mwaka la Arbaeen, ambalo linaweza kuongeza ufahamu wa kimataifa wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia kama vyombo vya habari vya kawaida vitaamua kufanya hivyo.

Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo maana yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu.

Baada ya kufa shahidi Imam Hussein (AS) mikononi mwa katili Yazid bin Muawiya, watu ambao walishangazwa na ukatili wa ukoo wa Ummaya walianza kuzuru kaburi lake kutoa heshima zao na tokea wakati huo hadi leo vizazi katika umma wa Kiislamu vimeendeleza utaratibu huo. Kila mwaka idadi ya wafanyaziara katika Siku ya Arabeen inaongezeka ambapo mwaka uliopita idadi hiyo ilivunja rekodi na kufika milioni 21.

Ziara hii ya kiroho ni dhihirisho la wazi la kujitolea na heshima isiyoyumba ambayo mamilioni ya waumini wanayo  kwa Imam Hussein (AS), inayowavuta kutoka kila kona ya dunia na kukusanyika kwenye mji wa Karbala nchini Iraq. Hapa, wafanyaziara au mazuwari hukusanyika kutoa heshima, kutafakari, na kupata faraja katika imani yao ya pamoja.

Vyombo vya habari vya kimataifa hupuuza Arbaeen

Ziara ya Arbaeen, katika fahari na ukubwa wake, inapaswa kuwa kivutio kisichozuilika kwa macho ya vyombo vya habari. Wakati mamilioni ya waumini, waliounganishwa na imani, wanapokusanyika ndani ya safu ya pekee ya ibada, ulimwengu unapaswa kushuhdia mandhari hii kwa mtazamo chanya.

Hata hivyo, vyombo vya habari vinavyodaiwa kuwa “haviegemei upande wowote” vinaonekana kuweka kupuuza tukio hili muhimu, na hivyo kuficha taswira yenye mvuto ya Uislamu wa madhehebu ya Shia.

Katika upendeleo wa vyombo vya habari, ukweli mara nyingi unakuwa mhanga.

Ni muhimu kuangazia simulizi hii iliyofichwa, kwa kuwa Uislamu wa Shia, kama imani yoyote, unajumuisha wigo wa imani na desturi za kipekee.

Kwa kushindwa kuakisi kiini Arbaeen, vyombo vya habari vya ulimwengu, hasa vya Magharibi, bila kukusudia vinaendeleza dhana potofu, na kuongeza pengo la kutokuelewana.

Watazamaji wa kimataifa wanakosa nini

Mkusanyko wa Arbaeen unaweza kuibua hisia ufahamu, kilele cha tahadhari kinachoangazia mafundisho na imani za Uislamu wa Shia. Vyombo vya habari vikiakisi tukio hilo muhimu basi vitaibua mchakato muhimu wa kuelimisha hadhira ya kimataifa kuhusu itikadi na maadili ambayo yanaunda msingi wa imani hii.

Ziara au safari ya Arbaeen inajitokeza kama fursa isiyo na kifani ya kueneza ujumbe mzito wa Uislamu wa madhehebu ya Shia, na kugusa maisha na nyoyo ambazo zingebakia bila kuguswa vinginevyo.

Tukitafakari tukio hili lenye mambo mengi, mtu anavumbua hazina ya njia zinazowezekana ambazo Arbaeen anaweza kutengeneza njia za kuelewa na kuhurumiana, na hivyo kurutubisha mbegu za ufahamu:

Kuvunja itikadi potofu: Ziara hii nasambaratisha dhana potofu zilizokita mizizi kuhusu Waislamu wa Shia huku pia ikiondoa dhana potofu na kukuza mtazamo sahihi zaidi wa imani. Mamilioni ya watu wanaposimama bega kwa bega, bila kujali asili, rangi au kabila, utando wa umoja uliofumwa miongoni mwa watu mbalimbali unaonyesha maelewano na ushirikishwaji katika moyo wa Uislamu wa Shia.

Mwanga wa amani

Mwanga wa amani: Ziara ya Arbaeen inasimama kama kielelezo hai cha amani na uvumilivu. Katika tukio hilo ulimwengu unashuhudia mchoro wa ubinadamu ambapo imani inakuwa daraja la ushirikiano, mazungumzo, na heshima, inayovuka migawanyiko ya kitamaduni na kidini.

Njia panda za kitamaduni: Tamaduni na kanuni zinazobadilika hupata msingi unaofanana katika ibada ya pamoja ambayo ni sifa ya Ziara ya Arbaeen. Kuchanganyika huku kwa mioyo na nafsi huchochea mazungumzo na uelewano, kuwezesha watu kutoka asili tofauti kufumbua maadili yaliyoshirikiwa na kufuta mipaka inayowatenganisha.

Kutafuta elimu: Kama Ziara ya Siku ya Arbaeen inavyoashiria, inawaalika watu, ndani na nje ya imani, kuzama katika Uislamu wa Kishia. Udadisi huu unaweza kuibua safari ya uchunguzi, ukawapa motisha watu kupata maarifa ya kina kuhusu imani, mazoea na mafundisho ya imani.

Wajibu wa vyombo vya habari kuziba mapengo

Kwa hakika, Safari ya Arbaien haisimami tu kama safari ya kuelekea mahali patakatifu, bali kama msafara wa imani, umoja, na utambuzi. Nguvu yake haipo tu katika nyayo zinazokanyaga njia ya kuelekea Karbala, lakini katika mawimbi ya mabadiliko inasambaa kote ulimwenguni.

Safari hii ya kila mwaka—safari ya nafsi na safari ya nyoyo—inaleta uhai katika mafundisho ya Uislamu wa Kishia, kuziba mapengo, kuvunja vizuizi, na kuwasha mwanga wa ufahamu unaong’aa zaidi ya upeo wa Karbala.

Hebu fikiria ulimwengu ambapo wakubwa wa vyombo vya habari walichagua kuelekeza lenzi zao kuelekea mikusanyiko mikubwa, ya amani wakati wa Arbaeen, kuonyesha umoja, uvumilivu, na hali ya kiroho ya kina ambayo imeenea kwenye tukio hili. Hatua hii inaweza kubainisha ubora wa Uislamu wa madhehebu ya Shia  na hatimaye kukuza maelewano na mazungumzo kati ya imani na tamaduni mbalimbali.

3484851

Habari zinazohusiana
captcha