IQNA

Diplomasia

EU yasema vitendo kama kuvunjia heshima Qur’ani ni kwa maslahi ya magaidi

22:15 - September 22, 2023
Habari ID: 3477634
NEW YORK (IQNA) - Vitendo kama vile kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu vinatumiwa na magaidi kwa maslahi yao, mkuu wa sera za kigeni wa EU alisema.

Josep Borrell alisisitiza haja ya kueneza uvumilivu katika jamii ili kupambana kikamilifu na ugaidi.

"Ili kukabiliana na chanzo cha ugaidi, ni lazima tuhusishe mashirika ya kiraia. Tunahitaji kuhimiza uvumilivu wakati tukishughulikia vitendo vya chuki, uchomaji moto wa Qur'ani, na kuwalenga walio wachache," Borrell alisema katika hotuba yake ya ufunguzi kabla ya Kongamano la Kimataifa la Kupambana na Ugaidi.

"Katika vitendo vyetu, kukabili ugaidi, na kuhusisha mashirika ya kiraia ni muhimu," alisema. "Hatuwezi kushughulikia ipasavyo sababu kuu za itikadi kali, au kuwarekebisha ipasavyo magaidi wa zamani bila kuendeleza jumuiya za kiraia, bila vyombo vya habari vilivyo huru na vya kuaminika au bila viongozi wa jumuiya."

Nafasi muhimu ya kiraia kwa madhumuni haya inaendelea kupungua katika sehemu mbalimbali za dunia, alisema. "Ndio maana lazima tufanye kila tuwezalo ili kubadilisha hali hii kote ulimwenguni," Borrell alisema.

Alisisitiza kuwa ili kupambana na ugaidi, dunia lazima iendeleze uvumilivu kwani ulimwengu unaona vitendo vya uchochezi na vitendo vya kutovumiliana na chuki mara kwa mara.

"Tunaona uchomaji wa Qur'ani, tunaona kulengwa kwa wafuasi wa dini au jamii zingine za wachache, kukichochea kutovumiliana na manung'uniko," alisema. "Hawa, mara kwa mara, wanatumiwa na magaidi kueneza itikadi zao potofu, kuajiri na kupeleka wahusika wa kigaidi."

Makundi yanayochukia Uislamu kaskazini mwa Ulaya katika miezi ya hivi karibuni yamekuwa yakitekeleza mara kwa mara uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu na majaribio kama hayo ya kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Waislamu, na hivyo kuzua hasira kutoka kwa nchi za Kiislamu na dunia nzima.

3485258

captcha