IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

EU: Kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ni 'Kutowajibika ya Watu Wasiowajibika'

18:23 - August 09, 2023
Habari ID: 3477408
BRUSSELS (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya alielezea kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kama "vitendo vya kutowajibika vya watu wasiowajibika".

Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao na wanahabari siku ya Jumanne, Peter Stano alisema mazungumzo na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) yataendelea "kuhimiza kuvumiliana na kuheshimiana" baada ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu hivi karibuni nchini Uswidi na Denmark.

Alieleza kuwa maafisa kutoka kamisheni na uwakilishi wa OIC wa Brussels wanafanya mazungumzo ya mara kwa mara "kuelewa hatua zinazofuata" baada ya matukio kadhaa ya uchomaji moto wa Qur'ani au unajisi kutokea hivi karibuni nchini Denmark na Uswidi.

Stano alisisitiza kwamba vitendo hivi "sio sera ya Umoja wa Ulaya" bali  ni vitendo vya kutowajibika vya watu wasiowajibika ambao wana nia ya kupanda mifarakano na shida, na kutugawanya kama jamii."

EU iko tayari kuendelea na majadiliano na OIC "kwa sababu huu ni wakati wa kusimama pamoja na kuimarisha juhudi zetu za kukuza uvumilivu na kuheshimiana," aliongeza.

Makundi yenye chuki dhidi ya Uislamu yamekuwa yakitekeleza mara kwa mara uchomaji moto wa Qur'ani Ulaya Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni, na hivyo kughadhabisha Waislamu na nchi za Kiislamu dunia nzima.

3484703

Habari zinazohusiana
captcha