IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Uchomaji moto Qur'ani una mizizi ya Kizayuni Inayolenga kuchochea chuki dhidi ya Uislamu

17:20 - August 10, 2023
Habari ID: 3477409
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano la Kiislamu la Iran (ICRO) ameyataja matukio ya hivi karibuni ya uchomaji moto wa Qur'ani barani Ulaya kuwa ni hatua ambazo zina mizizi ya Kizayuni.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano, Hujjatul Mohammad Mehdi Imanipour alisema kuwa, kwa kuzingatia matatizo yake ya ndani, utawala wa Kizayuni utawala wa Kizayuni unachochea vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Uchunguzi wa kina wa matukio ya hivi karibuni ya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu unadhihirisha kwamba mwenendo huu si kazi ya mtu mmoja au wawili bali una mizizi ya Uzayuni.

Hatua kama hizo zinalenga kuchochea chuki ya Uislamu duniani, Hujjatul Islam Imanipour aliongeza.

Vile vile ameashiria taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei kuhusu vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu na kusema ICRO pia imechukua hatua ikiwemo kuwaandikia barua viongozi wa kidini duniani ili wachukue hatua dhidi ya kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.

Afisa huyo alisema kwamba katika barua hii, kuandaa hati ya ulimwengu kuhusu haki za dini imependekezwa.

Katika wiki za hivi karibuni, kuchafuliwa kwa Qur'ani nchini Uswidi na Denmark kwa idhini ya serikali na ulinzi wa polisi kumezua hasira na shutuma nyingi kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Nchi hizo za eneo la Skandinavia  zinaruhusu vitendo hivyo viovu kutokea chini ya kivuli cha kile kinachoitwa uhuru wa kujieleza licha ya kulaumiwa vikali na mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu na hata mbele ya azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi uliopita.

 4161312

Habari zinazohusiana
captcha