IQNA

Waungaji mkono Palestina

Bunge la Afrika Kusini lapiga kura ya kufunga ubalozi wa utawala wa Israel

19:13 - November 22, 2023
Habari ID: 3477930
TEHRAN (IQNA)- Wabunge wa Afrika Kusini wamepiga kura ya kufunga ubalozi wa utawala wa kibaguzi wa Israel katika nchi hiyo.

 Bunge la Afrika Kusini Jumanne lilipiga kura ya kufunga ubalozi wa utawala huo ghasibu, kusimamisha nao uhusiano wa kidiplomasia na kumfukuza balozi  wa Kizayuni nchini humo.

Kabla ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni ilikuwa imetangaza kuwa, imemwita nyumbani balozi wake mjini Pretoria kwa ajili ya mashauriano kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya viongozi wa  Afrika Kusini.

Mwezi uliopita, Afrika Kusini ilivitaja vitendo vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza kuwa jinai na kumwita nyumbani balozi wake kutoka ardhi hizo zilizoghusibiwa.

Katika kukabiliana na jinai hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, Pretoria imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kumkamata Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa tuhuma za mauaji ya halaiki.

3486125

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini hapo awali alisema kuwa nchi yake imewasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ili kuchunguza jinai za kivita za utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Msimamo huo wa Rais wa Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni unakuja katika hali ambayo makumi ya maelfu ya wananchi katika mji wa Cape Town ulioko kusini magharibi mwa Afrika Kusini wamefanya maandamano ya kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za Israel hususan mauaji ya kimbari ya watoto wachanga huko Gaza.

 

Habari zinazohusiana
captcha