IQNA

Wasomi wa Kiislamu, wanaharakati wa Palestina wapinga uhusiano na Israel

11:14 - October 07, 2020
Habari ID: 3473238
TEHRAN (IQNA) – Wasomi wa Kiislamu na wanaharakati katika mirengo kadhaa ya Palestina wamelaani vikali mapatano ya kuanzishwa uhusiano baina ya Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu.

Katika kongamano la kimataifa ambalo lilifanyika katika Ukanda wa Ghaza, halikadhalika walisisitiza kuwa mpatano hayajafanikiwa kuvunja irada ya Wapalestina ya kupigania ukombozi wa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha walisema hatua ya kuanzisha uhusiano na Israel ni jinai isiyoweza kusameheka.

Washiriki kutoka nchi kadhaa za Kiislamu walishiriki katika mkutano huo kwa njia ya video.

Tarehe 15 mwezi wa Septemba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya rais wa Marekani, White House mjini Washington.  Hadi hivi sasa ulimwengu mzima wa Kiislamu bali hata baadhi ya nchi zisizo za Waislamu, kama Afrika Kusini zinalaani kitendo hicho cha kisaliti cha Bahrain na UAE. Hatua hiyo ya UAE na Bahrain imetajwa kuwa ni usaliti kwa kwa malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

3472752

Kishikizo: palestina israel
captcha