IQNA

Fikra za Kiislamu

Kuamrisha mema na kukataza mabaya humarisha mahusiano ya kijamii

21:14 - August 30, 2022
Habari ID: 3475704
TEHRAN (IQNA) – Moja ya njia za kuimarisha hisia za uwajibikaji miongoni mwa watu katika jamii ni kuamrisha mema na kukataza maovu.

Kama mojawapo ya mafundisho ya Kiislamu, kitendo hicho cha kuamriha mema na kukataza maovu kinajaribu kurekebisha tabia za watu binafsi huku pia kikiimarisha hisia zao za uwajibikaji kwa watu walio karibu nao ili wawazuie wengine kufanya mambo mabaya kwa kuwaalika na kuwapendekeza kufanya mambo mema.

Kuamrisha mema kunamaanisha kuamrisha au kuwaalika wengine kufanya mambo mema na kukataza maovu kunamaanisha kuwazuia wengine kufanya maovu. Hili si sawa na kuingilia maisha ya wengine, bali ni wajibu wa kijamii kuimarisha hisia za uwajibikaji wa kijamii.

Msisitizo ambao Uislamu umeweka juu ya kitendo hiki unalenga ukuaji wa wanadamu katika maisha yao ya kijamii. Ikiwa wanajamii watakuwa wasiojali wao kwa wao, uharibifu mkubwa, kama vile machafuko na ukosefu wa usalama, utawatishia.

Kuamrishana mema na kukataza maovu kutapelekea ukaribu wa watu binafsi baina ya wao kwa wao katika jamii kwa sababu wanahisi wajibu walio nao wao kwa wao; kadiri hisia hii inavyokuwa na nguvu, ndivyo uhusiano kati ya wanajamii utakavyokuwa thabiti zaidi.

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (Qur’ani Tukufu Sura At-Tawbah, aya ya 71)

Njia muhimu na kuu ya kuonyesha matendo mema ni kupitia tabia zetu wenyewe.

Maneno ya mtu anayewahimiza wengine kutenda mema lakini hafanyi anayosema hayatakuwa na athari. Kwa hiyo, ili iwe na ufanisi, ni lazima kwanza tujirekebishe wenyewe. Kwa mfano, nikiwaambia wengine tusitupe takataka, lakini tunafanya sisi wenyewe, sio tu maneno yetu hayatakuwa na athari bali hata tabia zetu zitatiliwa shaka.

Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii? (Qur’ani Tukufu Sura Baqarah, aya ya 44)

captcha