IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Iran yamkabidhi balozi wa Uswidi malalmiko kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

19:03 - July 21, 2023
Habari ID: 3477316
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemuita balozi wa Uswidi mjini Tehran kulalamikia hatua ya serikali ya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ya kuruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemkabidhi balozi huyo wa Uswidi mjini Tehran barua rasmi ya malalamiko na kumtaka aiwasilishe kwa serikali ya Stockholm.

Hii ni baada ya jeshi la polisi la nchi hiyo ya Ulaya kumpa idhini kwa mara nyingine tena raia wa Uswidi mwenye asili ya Iraq, Salwan Momika kuidhalilisha nakala ya Qur'ani Tukufu mjini Stockholm.

Momika hapo jana aliikanyaga na kuipiga mateke nakala ya Qurani Tukufu nje ya Msikiti mkuu mjini Stockholm, huku akipewa ulinzi na maafisa usalama wa nchi hiyo ya Ulaya.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katu Jamhuri ya Kiislamu haitoruhusu kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini kwa kisingizio chochote.

Kan'ani amesema kitendo hicho cha kichochezi na kinachogusa nyoyo na hisia za Waislamu bilioni mbili kote duniani hakipaswi kuhalalishwa kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

4156639

Habari zinazohusiana
captcha