IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Waislamu wahakikishe Uswidi inajuta kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu

18:55 - July 21, 2023
Habari ID: 3477315
TEHRAN (IQNA)- Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani serikali ya Uswidi kwa kuruhusu kuvunjiwa heshima tena Qur'ani Tukufu na amewataka Waislamu duniani kuchukua hatua za kuifanya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ijute kwa jinai yake hiyo.

Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khatami ameyasema hayo kwenye khutba za Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran na huku akiashiria kuvunjiwa heshima tena nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Uswidi jana Alkhamisi kwa kibali cha serikali na ulinzi kamili wa jeshi la polisi la nchi hiyo amesema, kama mwendawazimu amefanya upuuzi, sisi hatuwezi kuilaumu serikali, lakini kilichopo hapa ni kwamba jeshi la polisi la serikali ya Uswidi limempa ulinzi punguani huyo.

Sisi hatuogopeshwi na jinai hiyo kwani nafasi ya Uislamu na Qur'ani ni kubwa na tukufu mno, haiwezi kutetereshwa na upunguani wa watu kama hao, lakini pia ni wajibu wa Waislamu kusimama imara kulinda matukufu yao na ni wajibu wa mataifa ya Waislamu duniani kuchukua hatua ambazo zitaifanya serikali ya Uswidei ikome na ijute kufanya jinai kama hiyo.

Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameipongeza serikali na wananchi wa Iraq kwa hatua walizochukua zilizomlazimisha balozi wa Sweden kukimbilia kwenye ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kusisitiza kuwa, maadui wote wanapaswa kuelewa kwamba Qur'ani si Kitabu cha kuchezewa hata kidogo.

Vile vile amesema, miongoni mwa sifa tukufu za Mwenyezi Mungu, ni kutekeleza ahadi Zake na hakuna yeyote anayeweza kumfikia Allah katika utekelezaji wa ahadi Zake ambapo moja ya ahadi za Mwenyezi Mungu ni kwamba damu za mashahidi wanaoupigania Uislamu na matukufu yake, hazimwagiki bure.

Khatibu huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, matendo mema ya waokufa shahidi katika njia ya Allah hayapotei. Hata Qur'ani imesisitiza kuwa, mashahidi msiwaite ni watu waliokufa, kwani mashahidi wako hai zaidi kuliko sisi tulio hai hapa duniani na mfano wa wazi ni Imam Husain AS.

Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khatami pia amesema, karibu karne 14 zimepita tangu alipouawa shahidi Imam Husain AS lakini hadi leo hii na milele jina la mjukuu huyo wa Mtume na masahaba wake watoharifu litaendelea kukumbukwa kwa wema, ushujaa na uaminifu wao wa kupigiwa mfano.

4156746

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha