IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Kiongozi wa Hizbullah ataka nchi za Kiislamu kukata uhusiano wa kidiplomasia na Uswidi

20:40 - July 23, 2023
Habari ID: 3477327
BEIRUT (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameyataka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kukata uhusiano wao wa kidiplomasia na Uswidi (Sweden) baada ya kushuhudiwa matukio ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo.

Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, baada ya matukiio kadhaa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi msimamo wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu unapaswa kuwa ni kukata uhusiano wa kidiplomasia na taifa hilo la Ulaya.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha kwamba, Waislamu hawapaswi kuhadaika na hatua za kuomba radhi.

Nasrullah ameisifu hatua ya Iraq ya kumrejesha nyumbani balozi wake wa Uswidi na wakati huo huyo kumkufukuza nchini humo balozi wa Swedn na kueleza kwamba, hii ilikuwa hatua na ubunifu muhimu sana katika uga rasmi.

Kadhalika amesema, endapo Uswidi itaendelea na mwenendo huu, katika sheriia ya Kiislamu itakuwa nchi ambayo inaendesha chuki na vita dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Kafiri Salwan Momika, juzi Alkhamisi iliyopita alikivunjia tena heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu bilioni mbili dunia kwa ulinzi kamili wa jeshi la polisi la Sweden mjini Stockholm kama ambavyo pia aliivunjia heshima bendera ya Iraq mbele ya ubalozi wa nchi hiyo mjini humo.

Hatua hiyo imeendelea kulaaniwa katika pembe mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu huku baadhi ya mataifa yakitoa mwito wa kususiwa bidhaa za Uswidi sambamba na kukatwa uhusiano wa kidiplomasia na taifa hilo la bara Ulaya.

4157159

 

Habari zinazohusiana
captcha