IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Uswidi yakiri kukumbwa na mgogoro wa usalama baada ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

18:49 - September 01, 2023
Habari ID: 3477531
TEHRAN (IQNA)--Waziri wa Sheria wa Uswidi, Gunnar Stromer, ameonya kuhusu hali ya hivi sasa ya usalama nchini mwake na kusema kwamba hali yetu ni ya giza sana hivi sasa baada ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Waziri wa Sheria wa Uswidi amesema baada ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini humo kwamba Uswidi itaishi na hali ya giza ya usalama kwa muda usiojulikana.

Kwa upande wake, Frederick Hallström, Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Ugaidi ya Uswidi alionya jana Alkhamisi usiku kuhusu hali ya usalama ya nchi hiyo na kuongeza kuwa: Kuvunjiwa heshima mara kwa mara Qur'ani Tukufu nchini Uswidi kumebadilisha sura ya kimataifa ya nchi hiyo.

Amesema: "Picha za kuitovutikia adabu Qur'ani nchini Uswidi zinazotangazwa nje ya nchi hususan kwenye mitandao ya kijamii zinaongeza hatari za usalama na vitisho kwa nchi yetu."

Serikali ya Uswidi inaendelea kulaaniwa vikali, hasa na Ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kwa kisingizio cha eti uhuru wa kujieleza.

Katika miezi ya hivi karibuni, watu wenye misimamo mikali waliivunjia heshima Qur'ani Tukufu mbele ya Bunge la Sweden, mbele ya Msikiti Mkuu huko Stockholm na mbele ya balozi za Uturuki na Iraq mjini humo.

Katika nchi jirani ya Uswidi yaani Denmark, vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu vimefanywa pia na magenge yenye chuki na misimamo mikali dhidi ya Waislamu na Uislamu. Suala hilo limeifanya serikali ya Denmark kuwasilisha mipango wiki iliyopita ambayo kwa mujibu wake itavihesabu vitendo vya kuvunjia heshima maandishi ya kidini kuwa kosa la jinai.

Lakini Uswidi imesema tu inafikiria kufanyia marekebisho sheria zake lakini haijachukua hatua zozote za kufanikisha suala hilo.

3484995

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha