IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Supamaketi kubwa nchini Qatar yatangaza kususia bidhaa za Uswidi

22:40 - July 25, 2023
Habari ID: 3477340
QATAR (IQNA) -Supamaketi kubwa nchini Qatar imeondoa bidhaa zote za Uswidi kwenye rafu zake - na kutoa msimamo wa kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Supamaketi ya Souq Al Baladi imetangaza kuwa matawi yake yote hayatauza tena bidhaa zozote za Uswidi.
Klipu za video katika mitandao yakikamii zimeoonyesha wafanyakazi wakiondoa chokoleti maarufu ya Uswidi kwenye rafu. Ususiaji huo umekuja huku ulimwengu wa Kiislamu ukiendelea kulaani vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi.
Kitabu hicho kitakatifu kilichomwa au kuharibiwa wakati wa maandamano ya hivi karibuni ya umma katika mji mkuu wa Uswidi, na kusababisha hasira kote ulimwenguni.
Kukata uhusiano wa kisiasa na kibiashara kati ya nchi za Kiislamu na Uswidi sambamba kususia bidhaa za nchi hiyo pia inaweza kuwa sehemu ya kampeni kubwa ya Waislamu ya kupinga hatua ya serikali ya Uswidi ya kutoa kibali cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini humo. 
3484500

Habari zinazohusiana
captcha